Sunday, January 27, 2013

MUIMBAJI RACHEL SHARP AFANYA UTAMBULISHO WA ALBAM KWA WANAHABARI.

  Mc Event Rith Chuwalo akifanya utambulisho kwa waandishi pamoja na watangazaji waliofika.Kushoto Blogger Luphurise Lema,Blogger Nice Noel,Furaha Masinga kutoka Sibuka Tv.
Siku ya jana Tegeta yaliko makazi ya muimbaji Rachel Sharp kwa hapa Tanzania alifanya Utambulisho wa Albam yake mbele ya waandishi wa Habari.Mwanamuziki huyo alisema albam hiyo yenye jina la "Ni Mungu Wa Ajabu" ina jumla ya nyimbo kumi zilizo katika mfumo wa CD na nyimbo 8 zilizo katika DVD.
Katika Lisara yake iliyokua ndefu Rachel alisema DVD ya Albam yake amefanya sehemu tofauti tofauti ya Nchi yetu pamoja na Sweden yaliko makazi yake kwa sasa.Aliendelea kueleza Ipo haja ya watanzania Kuimba nyimbo zenye mahadhi ya Mdumange na Mdundiko ili kulinda radha halisi ya Kitanzania na Kuutangaza Muziki Wa Asili ya Kitanzania nje ya Mipaka Ya Tanzania.
Rachel akiwa ni Mama wa watoto wa wili waishio Sweden kwa sasa yupo katika likizo fupi nchini Tanzania ambako anafanya kazi ya mziki wa injili.  
 
  Uncle Jimmy akiwa na waandaaji wa vipindi kutoka Clouds Tv.Kulia ni Mudi Muzungu kushoto ni Faraja.
Mdogo wa mwisho wa Rachel
 Rachel akifanya utambulisho wa Baba mzazi na Mama mzazi.
 Upendo Kilahiro akifanya kweli
 Rachel akienda sawa katika uzinduzi wake
Rachel akisoma Lisala fupi
Master Prophet C.J. Machibya akiiyombea kazi ya dvd na Audio
Blogger Kyaruzi 
 Popote habari itakufikia kwa wakati huohuo.Papa the Blogger akitupia story.
Hapa sijui walikua wanafanya nini Rachel na King Chavala
 Blogger Luphurise Lema akiweka mambo sawa kwa kazi
 Mama Mzazi wa Rachel Sharp
 Kwa Makini Mr Machibya akiandika mawili matatu

 Papaa akifanya maojiano na Upendo Kilahiro pamoja na Rachel baada ya uzinduzi kumalizika.

Tuesday, August 28, 2012

"Napokea" Ya Jesca Honore Yatengenezwa na Exclusive Media ideo Ya Jesca Honore

Wimbo unaitwa NAPOKEA
Muimbaji ni JESSICA HONORE
Imetengenezwa na EXCLUSIVE MEDIA
Director wa video ni GODIE.
Mwanamuziki Wa injili ambaye aliibuka kinara wa Gospel Star Search kipindi hicho na ambaye emetengeneza Matangazo mengi Clouds FM kuliko Mwanamuziki mwingine wa Injili Tanzania Jesca Honore anategemewa kuachilia Wimbo wake "Napokea" Mwanzoni Mwa Mwezi Wa Tisa.
Waimbaji wengine wanakaribishwa kufanya video zenye ubora na ubunifu wa hali ya juu kwa gharama nafuu kupitia exclusive media.

Technical Team Ikiwa kazini kwenye shooting ya "Napokea"
Checks and Balance Wakati kazi inaendelea kama kawa
Director Wa Wimbo wa "Napokea" Godie akiwa Kikazi Zaidi
This is the Man, Mzee Wa Exclusive Media Sinza
Attention.....Action....
The Team
Jesca Honore
Twende kazi Action...........

HII NDIO STUDIO MPYA YA MUIMBAJI STEVEN WAMBURA "NIKO AMBAYE NIKO STUDIO"

Ni mara chache kusikia muimbaji wa mziki wa injili amefungua Studio au anamiliki studio yake.Kwa waimbaji wa mziki wa injili Tanzania ninaowafahamu wana studio ni Jackson Bent,Bonny Mwaitege,Flora Mbasha.

Leo katika Blog niko na Muimbaji wa miondoko ya Sebene alimaharufu Regra Steven Wambura.Yeye amefungua studio iliyoko Mwananyamala Kisiwani.Studio hii ina vyombo vilivyo kamilika na imeshafanya kazi na waimbaji wachache akiwemo Masanja Mkandamizaji.

Yako mengi utayapata hapa hapa kupitia Blog yako kuhusu ujio wa Studio hii.Na siku za usoni Steven Wambura anatarajia kuachia nyimbo Tatu kwa mfululizo

Twende sawa na matukio ya Picha ya Studio hii yenye jina la "NIKO AMBAYE NIKO STUDIO"
Produza Shushu akiaandaa mziki.
Steve Wambura akiwa na Prosper ndani ya studio ya Nikoambayenikostudio's
Prosper Mwakitalima.

Pastor Wambura akiwa na Masanja Mkandamizaji ndani ya Studio ya Nikoambayeniko walipokuwa wakifanya wimbo mpya ambao umetengenezwa na Produza Zakayo Shushu.Kaa mkao mzuri kupokea kolabo la Steve Wambura na Masanja Mkandamizaji.

BAADA YA KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI KWA MWAKA MMOJA UPENDO NKONE ARUDI TENA NA ALBAMU MPYA.

Kwa muda wa mwaka mmoja alikuwa kimya akisoma alama za nyakati na jinsi mziki unavyo kwenda.Kwa mara ya mwisho nilipo kutana naye aliniambia mziki umebadilika sana kwakua wapo waimbaji wapya ambao wamekuja na staili mpya ivyo yeye kama mkongwe anaangalia mziki unaelekea wapi.

Leo Blog ikiwa katika arakati zake imekutana na Albamu hii ya "UNIONGOZE YESU"Ikiwa ni Albamu ya 4 ya Mama Mchungaji Upendo Nkone.Albamu hii imeingia sokoni ikiwa na wiki moja.Ujio wa Albamu hii wenye nyimbo 11 ni ujio wenye maadhi ya Zuku,Sebene na Rumba.

Upendo Nkone mwaka Mwka 2008 alitamba na Albamu ya MUNGU BABA,2009-HAPA NILIPO,2010-ZIKO FAIDA KUKA NA MUNGU,Mwaka 2011 alikaa kimya akiangalia mziki wa injilii unaelekeaje.Na mwaka huu 2012 amekuja na UNIONGOZE YESU.
Muonekano wa juu wa kava ya Albamu hii.
Hizi ndizo nyimbo za Albamu yake.


Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign Centre, la Majumbasita UkongaJijijini Dar es salaam, Moses Magembe, amezindua kampeni maalumu ya maombi na maombezi, kwa muda wa majuma matano, ambapo kazi ya kuwafungua na uponyaji unaoambatana na matendo makuu ya nguvu za Mungu utaanza rasmi.

Akiongea katika Ibada ya hiyo maalum alisema kazi ambayo ameianza haitazimwa bali ameamua kuwasha moto katika siku za Jumatano,Alhamisi,Ijumaa na Jumapili kwa muda wa majuma yote matano fulululizo, hivyo ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na Vitongoji vyake, wakiwepo watu kutoka mikoa mbalimbali, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria maombezi hayo muhimu kwani katika kanisa hilo, masuala ya miujiza siyo kitu cha kushangaza bali watu wamekuwa wakitendewa na Mungu pasipo shaka.

Watu wengi walifunguliwa kupitia Ibada hiyo ya kipekee mara baada ya kuombewa na mpakwa mafuta wa huyo wa Bwana, Mchungaji Moses Magembe ambaye ameamua kujitoa mhanga, kuieleza kweli mbele ya jamii ya Wakristo, na kuipinga imani potofu zilizozagaa nchini, huku akiamua kuendesha Operation maalumu, ya maombezi kupitia jina kuu la BWANA Yesu Kristo.

Friday, July 13, 2012

Sage Moonblood Stallone, the 36-year-old son of Sylvester Stallone who starred alongside his father in "Rocky V," was found dead in his Hollywood apartment on Friday. The New York Post confirmed his passing with his attorney George Braunstein. Sources tell The Post that he likely died of an overdose of pills, and that a representative of the LAPD stated, "There is no suspicion of foul play or criminal activity."

Sage Stallone was Sylvester Stallone's eldest son from his first marriage to Sasha Czack (they divorced in 1985). Sage is survived by his brother Seargeoh, and his three half-sisters Sophia, Sistine, and Scarlet.

Sage made his film debut playing Robert Balboa, Rocky's son, in 1990's "Rocky V" when he was 14 years old. The film was both a critical and financial disappointment, with Sylvester Stallone telling The Sun in 2010 that the reason he made the sequel was "I'm greedy — what can I tell you... It was a mistake because the audience didn't want to see the downside of the character. They wanted him to remain on top."

Sage also appeared with his father in 1996's "Daylight," but that year also saw him give up acting to be one of the co-founders of Grindhouse Releasing. Along with his partner, Oscar-winning film editor Bob Murawski, Sage Stallone's company restored and re-released forgotten exploitation films from the 1970s and '80s. Grindhouse Releasing partnered with Quentin Tarantino to bring Lucio Fulci's horror film "The Beyond" to screens in 2010.

Sylvester and Sage Stallone in 'Rocky V' (Photo: Everett Collection)Reportedly, Sage turned down the chance to reprise his role of Rocky's son in 2006's "Rocky Balboa" to focus on his burgeoning career and a director and producer. The character was played in the sixth film by Milo Ventimiglia (TV's "Heroes").

Sylvester Stallone has not yet released a comment. Just yesterday the elder Stallone appeared at Comic-Con International in San Diego, CA to promote his upcoming action film "The Expendables 2." Stallone was joined on stage by Arnold Schwarzenegger, who makes his first appearance since leaving the office as governor of California in the movie.

Wednesday, May 16, 2012

John Lisu azidi kufanya kweli Nairobi-Kenya

John Lisu azidi kufanya kweli Nairobi Kenya katika Tuwa ya Jehova Yu Hai,Apo jana akiwa katika Kanisa la International Christian Centre Church Mombasa rd,Nairobi Kenya maelfu ya watu wamebarikiwa na Tuwa hiyo.

John Lisu akifanya kweli ndani ya ICC Nairobi.

John Lisu