Tuesday, August 28, 2012

HII NDIO STUDIO MPYA YA MUIMBAJI STEVEN WAMBURA "NIKO AMBAYE NIKO STUDIO"

Ni mara chache kusikia muimbaji wa mziki wa injili amefungua Studio au anamiliki studio yake.Kwa waimbaji wa mziki wa injili Tanzania ninaowafahamu wana studio ni Jackson Bent,Bonny Mwaitege,Flora Mbasha.

Leo katika Blog niko na Muimbaji wa miondoko ya Sebene alimaharufu Regra Steven Wambura.Yeye amefungua studio iliyoko Mwananyamala Kisiwani.Studio hii ina vyombo vilivyo kamilika na imeshafanya kazi na waimbaji wachache akiwemo Masanja Mkandamizaji.

Yako mengi utayapata hapa hapa kupitia Blog yako kuhusu ujio wa Studio hii.Na siku za usoni Steven Wambura anatarajia kuachia nyimbo Tatu kwa mfululizo

Twende sawa na matukio ya Picha ya Studio hii yenye jina la "NIKO AMBAYE NIKO STUDIO"
Produza Shushu akiaandaa mziki.
Steve Wambura akiwa na Prosper ndani ya studio ya Nikoambayenikostudio's
Prosper Mwakitalima.

Pastor Wambura akiwa na Masanja Mkandamizaji ndani ya Studio ya Nikoambayeniko walipokuwa wakifanya wimbo mpya ambao umetengenezwa na Produza Zakayo Shushu.Kaa mkao mzuri kupokea kolabo la Steve Wambura na Masanja Mkandamizaji.

No comments:

Post a Comment