Wednesday, April 25, 2012
Askofu Gwajima Ziarani Jijini London
Askofu Josephat Gwajima akihubiri jijini London Mwaka jana mwishoni |
Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Glory f Christ Tanzania anatarajia kuwepo jijini london kuanzia jumapili
hii ya tarehe 29 hadi tarehe 6 ya mwezi wa tano.kwa yeyote ambaye angependa
kukutana na mchungaji kwa ajili ya maombi na ushauri basi anatakiwa kupiga simu
namba
0742 7532044 au
07429667095
ili kupanga siku na muda ambao
angekutana na mchungaji.
Pamoja na hayo mchungaji atakuwa kwenye tawi la kanisa lake jumapili zote mbili kwa yeyote ambaye angependa kufika afuate anuani hii
Pamoja na hayo mchungaji atakuwa kwenye tawi la kanisa lake jumapili zote mbili kwa yeyote ambaye angependa kufika afuate anuani hii
Glory of christ ministries
international,
langham road,Tottenham,
London, N15 3RB.
Kwa Maelezo zaidi unaweza piga simu
kwenye namba tajwa hapo juu.
Paty attah na Eucharia Anunobi Ma-staa wa Nigeria waliompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha Yao
Paty Attah |
Paty attah ni raia wa Nigeria na
mmoja kati ya wakongwe wa tasnia ya filamu nchini humo , kwa miaka ya hivi
karibuni, Paty amempokea kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Baada ya
kuokoka, amekuwa akijituma katika kuwarudisha watu wengi kwa kristo kupita njia
mbalimbali pamoja na kushare maneno ya Mungu katka wall yake ya Facebook na
Twitter
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya
nchini Nigeria Paty kwa sasa anaishi jijini Humburg nchini Ujerumani na tofauti
na utumishi, Paty ni muigizaji wa Filamu kazi ambayo anaiendeleza nchini humo
.Pamoja na hayo pia ni mwanamitindo na Mwanamuziki. Paty mpaka sasa ameshacheza
zaidi ya filamu arobani zikiwemo Secret Fantasy, Final Spirit of Love, Fools in
Love, More than Gold, Only Love pamoja na Songs of Sorrow.
Eucharia Anunobi |
Kama kuna watu ambao waliwahi
kuushangaza uma wa wanigeria kwa kauli zao kuwa wameamua kuokoka basi Eucharia
Anunobi ni mmoja wao,Eucharia maarufu
kama UK, alikuwa ni mmoja wa ma-staa wa Nollywood waliojulikana sana hasa kwa
mtindo wake wa kuvaa nguo huku sehemu kubwa ya kifua chake ikiwa wazi.
Kwa sasa UK ameokoka na amekuwa akihubiri na
kumshuhudia Yesu pasipo kificho.Kuna habari za hivi karibuni zinasema ameamua
kuwa mchungaji na amesimikwa rasmi kwa kazi hiyo hivyo kwa sasa anachunga
kanisa lake.Eucharia alipata nafasi ya kuhubiri wakati wa kusimikwa u-shemasi
mbunifu wa mitindo na muigizaji nguli nchini humo Clarion Chukwura’s
Tuesday, April 24, 2012
ZIARA YA UPENDO KILAHIRO NCHINI CANADA YAANZA KWA MAFANIKIO WATU WATATU WAMPOKEA YESU
Upendo Kilahiro akimsifu Mungu. |
Mwimbaji nyota wa gospel nchini Tanzania Upendo Kilahiro ameweza
kupokelewa vyema nchini Canada huku tamasha lake la kwanza kufanyika
jijini Ottawa ndani ya kanisa la Christ Chapel Bible kufanyika kwa
mafanikio ikiwa ni pamoja na watu watatu kukabidhi maisha yao kwa Yesu
na mwengine akipokea uponyaji.
Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kwa ajili ya kukusanya fedha
za umaliziaji wa shule ya watoto yatima ya mkoani Morogoro nchini
Tanzania iitwayo Dayspring Orphanage boarding school ambayo inafadhiliwa
na kanisa hilo,ambapo watu wengi walihudhuria wakiwemo kutoka makanisa
ya jirani kama River Jordan Community kwakuwa ni kawaida makanisa jirani
kusaidiana na kuwa pamoja kwenye matukio kama hilo,tamasha hilo
liliongozwa na viongozi wa kanisa hilo akiwemo Bishop Afolabi,Peter
Mwaiteleke huku wageni rasmi walikuwa maafisa ubalozi wa Tanzania nchini
humo pamoja na Dada Niku Kyungu Mordi na mumewe ambao hufanya huduma ya
kuhubiri huko Maryland Marekani.
Upendo aliimba nyimbo mbalimbali na kuwabariki watu waliofika katika
tamasha hilo,mwimbaji huyo ambaye si mara yake ya kwanza kuwa nchini
Canada,pia mwishoni mwa mwaka jana yeye pamoja na waimbaji wenzake
Christina Shusho na Upendo Nkone walikuwa nchini Marekani kwa ziara ya
kumsifu Mungu. atakuwa nchini humo kwa ziara ya mwezi mmoja,huku
mwimbaji mwingine Flora Mbasha na mumewe wakiwa nchini Marekani kwa
ziara ya kumsifu Mungu.
Bishop Afolabi akimkaribisha Upendo Kilahiro kwa ajili ya kumsifu Mungu. |
Hakika ngome zilianguka. |
Mchungaji Peter Mwaitekele akipozi na Upendo kwa ajili ya picha. |
Dada Edith Mwita mdau mkubwa wa gospel VIPAJI HALISI Canada ambaye ndiye aliyefanikisha habari hii akiwa kwenye picha ya pamoja na Upendo Kilahiro. |
Zainabu mwanadada aliyekata shauri na kumpokea Kristo mwaka uliopita akipozi na Upendo. |
Watoto waliguswa na uimbaji wa Upendo wakaomba sign yake. |
Dada Edith Mwita,Zainabu pamoja na wanaigeria wakipozi kwa ajili ya kupata picha. |
Hakika ilikuwa siku ya furaha . |
Friday, April 20, 2012
''AHADI ZAKE'' WA MARION SHAKO WIMBO ULIOTOLEWA NENO LA KINABII KABLA HATA HAUJATUNGWA''
Marion Wyali Shako. |
''Nafsi yangu usichoke roho yangu msifu Bwana aliahidi atatenda,mtumainie Bwana,ahadi zake ni za milele akiahidi atatenda,roho yangu nafsi yangu mtumaini Bwana.
Kama mvua ishukavyo toka mbinguni kwenye ardhi na neno lake kwa kinywa chake halitarudi bure,litatimiza ahadi zake litatenda alivyosema aliahidi atatenda mtumainie BWANA''
Hayo ni maneno katika beti la kwanza na kiitikio cha wimbo ''AHADI ZAKE'' wimbo ambao umetoka takribani miaka minne iliyopita lakini ukiendelea kubariki na kugusa watu wengi mpaka leo kupitia mwimbaji wake na mtunzi wa wimbo huo mwanadada Marion Wyali Shako,ambaye kitaaluma kasomea mambo ya utawala(Administrative Assistant)akiwa mwajiriwa katika moja ya ofisi huko Mombasa nchini Kenya.
Katika taarifa yake ambayo aliwahi kuitoa kupitia Wapo Radio Fm akihojiwa katika kipindi cha ''Safari ya jioni'' alisema wimbo wa AHADI ZAKE ambao upo ndani ya album yake ya ''MSAADA WANGU'' alipewa neno la kinabii na nabii Teresia Wairimu kwamba Mungu atampa wimbo utakaobadilisha maisha yake na watu wengine,wakati anapewa unabii huo alikuwa katika hali ya uhitaji sana na album yake hiyo mpaka anaifanikisha kuirekodi ni Mungu mwenyewe alimsimamia kwani alimaliza salio lake lote alilokuwa nalo na pia alipitia mapito magumu sana.
Lakini kama mtumishi wa Mungu alivyompa unabii ni kweli ikatimia wimbo wa ''AHADI ZAKE'' umebadilisha maisha yake na watu wengi sio Kenya tu bali sehemu mbalimbali duniani
Marion alipotembelea nchini Uingereza mwaka 2009,akiwa katika pozi na masanamu ya familia ya Prince Charles,mkewe Camilla pamoja na watoto wake Prince William pamoja na prince Harry. |
No comments:
Post a Comment