ISAYA 40: 1-4, ISAYA 49:8-10, AYUBU 7:1-7
Mtumishi wa Mungu Mch.Meshark Mhini |
Faraja kwa watakatifu ni ujumbe wa matumaini, Kama ilivyotabiriwa na nabii isaya kuwa lipo tumaini kwa Mungu vile vile tukipata mifano mbalimbali kutoka kwenye biblia kuna watu walipitia katika maisha na mapito magumu sana kama ayubu, na pale alipokua akisema na Mungu wake kama ukisoma kuanzia mstari wa pili katika kitabu cha ayubu 7, tunaona jinsi mtu huyu alivyoteseka lakini Mungu alimpa neno la faraja na matumaini.
Washirika wakiwa kanisani Mwenge |
Mpiga ngoma maarufu Lumbaeli |
Wanamuziki wa mwenge, Joseph Ndidi na Shedrack Mboma |
Neno la Mungu linatukumbusha kuwa leo lipo tumaini, Bwana Yesu anataka kushughulika na matatizo ya maisha yako,kazini, shuleni, nyumbani, kwenye biashara yako nk. yeye ni yule yule jana leo na hata milele. Kama ilivyokuwa kwa ayubu Bwana yesu atatenda Muujiza kwako leo maana yeye ni Mungu mkuu hajawahi kushindwa na ana uweza wa ajabu, kinachotakiwa ni kumtii tu.
No comments:
Post a Comment