BREAKING NEWZ: POLISI WALIPUA MABOMU KUTAWANYA WAANDAMANAJI KESI YA KUCHOMA KURAN MWANZA.
Jumla ya watuhumiwa wanne wanadaiwa kushirikiana kuchoma Korani, asubuhi ya leo wamefikishwa mahakamani hapa kujibu mashtaka dhidi yao katika kesi inayotajwa kuahirishwa zaidi ya mara nne sasa kutokana na kuhofia usalama wa watuhumiwa.
Watuhumiwa wanaohusishwa na kesi hiyo ni waumini wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG) ni Tumaini Jumanne (30) ambaye ni mwalimu wa Biblia, Petro Mashauri (29) mfanyabiashara, Dickson Magai (30) mfanyabiashara na mwanamke pekee, Kalista Mlomo ambaye ni mkulima.
Wakikabiliwa na mashitaka matano ambayo ni kula njama, kufanya kusanyiko lisilo halali, kuingia kwa jinai nyumbani kwa Husna Hamis na kuharibu mali, pamoja na lile linalozungumzwa zaidi la kudhalilisha dini kwa kuchoma moto kitabu cha Korani Tukufu.
Kesi imesababisha barabara kufungwa kwa muda hadi hali itakapo tulia.
Si biashara tena bali msaada kukosha macho kwa maji ya kahawa.
Askari wa jeshi la polisi wakifanya doria eneo la mahakama.
Kutokana na hatua ya kufunga barabara watu wamelazimika kutembea kwa miguu nao polisi wakipiga marufuku kusanyiko la aina yoyote kwenye eneo husika.
No comments:
Post a Comment