Tuesday, August 28, 2012

BAADA YA KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI KWA MWAKA MMOJA UPENDO NKONE ARUDI TENA NA ALBAMU MPYA.

Kwa muda wa mwaka mmoja alikuwa kimya akisoma alama za nyakati na jinsi mziki unavyo kwenda.Kwa mara ya mwisho nilipo kutana naye aliniambia mziki umebadilika sana kwakua wapo waimbaji wapya ambao wamekuja na staili mpya ivyo yeye kama mkongwe anaangalia mziki unaelekea wapi.

Leo Blog ikiwa katika arakati zake imekutana na Albamu hii ya "UNIONGOZE YESU"Ikiwa ni Albamu ya 4 ya Mama Mchungaji Upendo Nkone.Albamu hii imeingia sokoni ikiwa na wiki moja.Ujio wa Albamu hii wenye nyimbo 11 ni ujio wenye maadhi ya Zuku,Sebene na Rumba.

Upendo Nkone mwaka Mwka 2008 alitamba na Albamu ya MUNGU BABA,2009-HAPA NILIPO,2010-ZIKO FAIDA KUKA NA MUNGU,Mwaka 2011 alikaa kimya akiangalia mziki wa injilii unaelekeaje.Na mwaka huu 2012 amekuja na UNIONGOZE YESU.
Muonekano wa juu wa kava ya Albamu hii.
Hizi ndizo nyimbo za Albamu yake.


No comments:

Post a Comment