Sunday, January 27, 2013

MUIMBAJI RACHEL SHARP AFANYA UTAMBULISHO WA ALBAM KWA WANAHABARI.

  Mc Event Rith Chuwalo akifanya utambulisho kwa waandishi pamoja na watangazaji waliofika.Kushoto Blogger Luphurise Lema,Blogger Nice Noel,Furaha Masinga kutoka Sibuka Tv.
Siku ya jana Tegeta yaliko makazi ya muimbaji Rachel Sharp kwa hapa Tanzania alifanya Utambulisho wa Albam yake mbele ya waandishi wa Habari.Mwanamuziki huyo alisema albam hiyo yenye jina la "Ni Mungu Wa Ajabu" ina jumla ya nyimbo kumi zilizo katika mfumo wa CD na nyimbo 8 zilizo katika DVD.
Katika Lisara yake iliyokua ndefu Rachel alisema DVD ya Albam yake amefanya sehemu tofauti tofauti ya Nchi yetu pamoja na Sweden yaliko makazi yake kwa sasa.Aliendelea kueleza Ipo haja ya watanzania Kuimba nyimbo zenye mahadhi ya Mdumange na Mdundiko ili kulinda radha halisi ya Kitanzania na Kuutangaza Muziki Wa Asili ya Kitanzania nje ya Mipaka Ya Tanzania.
Rachel akiwa ni Mama wa watoto wa wili waishio Sweden kwa sasa yupo katika likizo fupi nchini Tanzania ambako anafanya kazi ya mziki wa injili.  
 
  Uncle Jimmy akiwa na waandaaji wa vipindi kutoka Clouds Tv.Kulia ni Mudi Muzungu kushoto ni Faraja.
Mdogo wa mwisho wa Rachel
 Rachel akifanya utambulisho wa Baba mzazi na Mama mzazi.
 Upendo Kilahiro akifanya kweli
 Rachel akienda sawa katika uzinduzi wake
Rachel akisoma Lisala fupi
Master Prophet C.J. Machibya akiiyombea kazi ya dvd na Audio
Blogger Kyaruzi 
 Popote habari itakufikia kwa wakati huohuo.Papa the Blogger akitupia story.
Hapa sijui walikua wanafanya nini Rachel na King Chavala
 Blogger Luphurise Lema akiweka mambo sawa kwa kazi
 Mama Mzazi wa Rachel Sharp
 Kwa Makini Mr Machibya akiandika mawili matatu

 Papaa akifanya maojiano na Upendo Kilahiro pamoja na Rachel baada ya uzinduzi kumalizika.

No comments:

Post a Comment