Tuesday, August 28, 2012

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign Centre, la Majumbasita UkongaJijijini Dar es salaam, Moses Magembe, amezindua kampeni maalumu ya maombi na maombezi, kwa muda wa majuma matano, ambapo kazi ya kuwafungua na uponyaji unaoambatana na matendo makuu ya nguvu za Mungu utaanza rasmi.

Akiongea katika Ibada ya hiyo maalum alisema kazi ambayo ameianza haitazimwa bali ameamua kuwasha moto katika siku za Jumatano,Alhamisi,Ijumaa na Jumapili kwa muda wa majuma yote matano fulululizo, hivyo ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na Vitongoji vyake, wakiwepo watu kutoka mikoa mbalimbali, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria maombezi hayo muhimu kwani katika kanisa hilo, masuala ya miujiza siyo kitu cha kushangaza bali watu wamekuwa wakitendewa na Mungu pasipo shaka.

Watu wengi walifunguliwa kupitia Ibada hiyo ya kipekee mara baada ya kuombewa na mpakwa mafuta wa huyo wa Bwana, Mchungaji Moses Magembe ambaye ameamua kujitoa mhanga, kuieleza kweli mbele ya jamii ya Wakristo, na kuipinga imani potofu zilizozagaa nchini, huku akiamua kuendesha Operation maalumu, ya maombezi kupitia jina kuu la BWANA Yesu Kristo.

No comments:

Post a Comment