Tuesday, August 23, 2011

Christina Shusho aibuka Mwanamuziki Bora wa Kike wa Nyimbo za Injili Afrika mashariki na Kati



Mwana mama kutoka Tanzania Christiana Shusho ameibuka kuwa mwanamuziki Bora wa Kike wa Muziki wa Injili kwa nchi za Afrika mashariki na kati katika Tuzo ziitwazo East Afrika Music Awards (EAMA`S) zilizofanyika jumamosi iliyopita jijini Nairobi nchini Kenya.

Katika tuzo hizo Tanzania Tuliwakilishwa na wanamuziki wa injili wapatao wawili ambao ni Christina Shusho, Upendo Nkone ambao kwa pamoja walikuwa wakiwania Tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike wa injili kwa Afrika mashariki . Pia kwa upande wa Makundi tuliwakilishwa na Mwanza Gospel Choir ambao wao walikuwa wanawania tuzo ya Kundi bora la muziki wa injili kwa Afrika mashariki.

Christina Shusho
Mashindano hayo yaliyojumuisha aina mbalimbali ya muziki ukiwemo wa injili huku yakishirikisha jumla ya nchi nane ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Sudani pamoja na Kongo Kinshasa(DRC) na kuonyeshwa moja kwa Moja na Kituo cha ITV.


Yafuatayo ni majina ya washiriki waliokuwa wakiwania Tuzo hizo na wenye rangi ya nyekundu ndio washindi huku kwa upande wa wanaume walipatikana washindi wawili.

Gospel Category

Best Male
1. Cedric Bangy - "Segneur" - Burundi.
2. Dominique Ashimwe - "Nditabye" - RWANDA
3. Dawit Getachew - "Etebikihalehu" - ETHIOPIA
4. Wiseye Willie - "Buye Gigitare" - BURUNDI


Best Gospel Female

1. Christina Shusho - "Unikumbuke" - TANZANIA
2. Gaby - "Amahoro" - RWANDA
3. Alice Kamande - "Upendo Ule ule" - KENYA
4. Upendo Nkone - "Haleluyah Usifiwe" - TANZANIA


Best Gospel Group

1. Nef Thalem Assegid - " Nebse" - ETHIOPIA
2. Mwanza Gospel Choir -Nivema" - TANZANIA
3. B.M.F - "I live for you" - KENYA


Best Gospel Collabo

1. Emmy Kosgei ft. Lynn. "Omegeu Rerein" - KENYA
2. Mbuvi Ft. Kambua - "Kivevelo" - KENYA


Jose Chameleone Returns to Catholic Religion for the Good of His Family

Kutana na DOUBLE E Sisters Mabinti wanaofanya Vizuri kwenye Tasnia ya Muziki wa Injili



Evelyn na Esther wanaounda kundi la DOUBLE E Sisters wakiongea mara baada ya kunyakua Tuzo ya KUNDI BORA la Muziki wa injili 2011

Kila kukicha muziki wa kiroho ama wa injili wigo wake umekuwa ukipanuka siku hadi siku, na kupeleka wasanii wa muziki huo kungezeka kila kukicha, kundi la muziki wa injili liitwalo Double E ni moja ya kasi ya zao hilo,Kwa sasa kundi hilo linafanya vyema katika anga za injili nchini Tanzania. Kufanya vyema huko kumepelekea kundi hilo kupata tuzo ya Tanzania Gospel muziki Award kwa kuibuka na tuzo ya kundi Bora la mwaka 2010/2011.


Hosanna Inc imefanikiwa kufanya mahojiano kuhusiana na mambo mbalimbali hususani suala zima la uimbaji wa nyimbo za injili na namna walivyofanikiwa kuinyakua tuzo hiyo na kuacha wengine wakiwa na butwaa.


Kundi hilo linaundwa na wakina dada wawili ambao ni watoto wa familia moja, Ester na Evelyn Benard, HI ilianza na Ester ambaye alianza kwa kueleza kuwa yeye Ester Benald Kingo alizaliwa miaka 21 katika hospital ya Mount Meru mkoani Arusha na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya uhuru iliyopo Arusha na sekondari akajiunga Kenton secondary School iliyopo jijini Dar es saalam na baadae akaenda nchini Uganda akajiunga na shule ya `Nai High School;

DOUBLE E SISTERS Wakipokea TUZO pale Diamond Jubelee mapema mwaka huu

Kwa upande wa Eveline Benald Kingo ambaye ni dada yake Ester yeye alizaliwa miaka 24 iliyopita jijini Dar es salaam, na kupata elimu yake jijini Dar es salaam na baadae mjini Arusha na kwenda nchini Uganda.

Akieleza jinsi walivyoanzisha kundi lao la Double E, Ester ansema kuwa kundi hilo limetokana na yeye mwenyewe kwa vile alikuwa anapenda sana kuimba na kujikuta akimuambukiza dada yake, hivyo ikapelekea wao kuamua kuunda kundi hilo lilijulikana kwa jina la Double E, yaani Ester na Eveline.

‘‘Namshukuru sana Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo kwa sababu yeye ndiye aliyekusudia kundi letu liwepo, kiufupi mimi nilikuwa napenda kuimba tangu nilikuwa na miaka saba, wakati huo nilikuwa naimba Sunday school na baadaye nikaendelea na kuanza kutunga tunga nikaona ni vyema nimshirikishe na dada yangu ambaye kweli alikubali na kujikuta tukifanya pamoja,’’anasema Ester.

Kwa upande wa Eveline ambaye yeye ni mkubwa, anasema kwanza anammshukuru Mungu kwa namna ambavyo kundi lao limefanikiwa kupokelewa vyema ndani ya jamii na kujikuta likipata mafanikio kila kukicha, Eveline anaongeza kuwa mdogo wake ndiye aliyepelekea yeye aingie kwenye fani ya kuimba, na kweli alibaini kuwa hana namna hivyo aliingia kwenye fani ya uimbaji na kufanya vyema.

Evelyn na Esther wakiwa na Mama yao mzazi ambaye ni mzee wa kanisa katika kanisa la Eagt Mito ya Baraka
Double E wenye ndoto ya kuwa na studio yao ya kurekodi Video na Audio, pia ni wanafunzi wa kozi ya IT . Evelyn aliiambia Hosanna Inc kuwa moja kati ya changamoto kubwa waliokutana nayo ni kukatishwa Tamaa, alisema wengi waliwaambia kuwa nyie hamuwezi kuimba labda mjaribu kitu kingine lakini kwa kuwa walimjua wanayemtumikia hivyo hawakukata tamaa.


Mpaka sasa kundi hilo la Double E, limefanikiwa kutoa albamu yao ya Kwanza iitwayo NAPAMBANA na inafanya vyema katika soko la mziki wa injili, Album hiyo inajumuisha nyimbo zipatazo 10 ikiwemo `Napambana, it`s over, Yesu yupo, Umeniumba, Natangaza, yatima, pamoja na `Wamtumainio Bwana ambazo zote wameziekodi studio ya Baucha iliyoko maeneo ya stesheni jijini Dar es salaam. Mpaka sasa Double E wamefanikiwa kurekodi video ya wimbo wao uitwao `Napambana` unaofanya vyema katika muziki wa injili.

Kushoto ni Evelyn Benard na kulia kwake ni Esther Benard
Kwa sasa wanajiandaa kurekodi albamu ya pili ambayo wamekwisha ikamilisha, wanasema kuwa wanatarajia ifikapo mwishoni mwa mwaka huu itakuwa tayari iko sokoni. Mabinti hawa wameshirikishwa katika nyimbo za wanamuziki mbalimbali akiwemo Anaclara pamoja na Flora Okevo, pia wameingiza sauti katika wimbo uitwao Umenichagua uliomo katika album mpya ya Mtumishi Emmanuel Mgaya.

Wanamuziki hao wametoa ujumbe kwa waimbaji wenzao kuwa wasonge mbele kihuduma na wajitahidi kuwasaidia waimbaji wachanga wanaochipukia ili nao waweze kusonga mbele zaidi, aidha walimalizia kwa kutoa shukrani kwa familia yao ambayo imekuwa ikiwapa sapoti kubwa na pia kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao wamekuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanatimiza ndoto zao katika uimbaji.



Their Favorite Gospel Group: Marry Marry
Best Hymn: Chakutumaini Sina
Favorite Bible Verse: Methew 18:18-20
Their Favorite Gospel Artist: Ephraim Sekeleti
Favorite Colour: Chocolate


Uskose kufuatilia Hosanna Inc jumanne ijayo tutakuwa na mtumishi wa Mungu Denis Massawe Mtanzania afanyaye huduma nchini Uingereza.


RIOT Event Yafana



Hatimaye lile Tamasha la Muziki wa Injili linalowahusisha vijana zaidi lililofahamika kama RIOT limefanyika jijini Dar es salaam siku ya jumapili iliyopita wakati uzinduzi rasmi wa RIOT ulifanyika siku ya jumamosii mlimani City ikiwa ni siku moja kabla ya Tamasha lenyewe.

Mratibu wa Tamasha hilo Bro Isack Malonga pamoja na Timu nzima ya Tehilah Ministry walifanya kazi kubwa kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.Fuatana nasi ujionee kwa kifupi yaliyojiri.


Ni Mara chache sana kuona stage kama hizi zikitumika katika muziki wa injili nchini Tanzania

On tha Way From Uganda wanaitwa Soul 5 wakiwakilisha


Joy mwanzo Mwisho
Umati wa watu waliohudhuria RIOT Event pale Mbezi

Kutoka kulia ni Apostle Onesmo Ndegi, Isack Malonga pamoja na Benjamin Dube kutoka Afrika ya Kusini

Pastor Benjamin Dube akimuombea Isaack Malona "Hata Mama Yako hakujua amezaa Zawadi ya Namna gani, Watanzania hamuwezi Jua mnazawadi ya Namna gani, What I know, your Blessings are Connected to This Man Of God Isaac" Hayo ni baadhi ya Maneno ya Pastor Benjamin Dube akiongea kwa ajili ya Isaac.


No comments:

Post a Comment