Monday, August 22, 2011

Hivi ndivyo Ilivyokuwa Jijini Dar Kwenye R.I.O.T

Raising The Standard........R.I.O.T Festival Episode One Sizon One Its Far Above....Haipimiki

Historia imeandikwa kwa mara ya kwanza katika Kizazi cha karne ya 21 hapa Tanzania, Haijawahi kutokea na Wala Sijawahi kuona wala kusikia hapa Tanzania kwa miongo Kadhaa niliyoishi sijawahi kuona kile ambacho Kimezaliwa Leo katika Ukumbi wa Mlimani City.

"Hakuna Kazi Ngumu Kama Kizazi Kilichopita Kifikra Kikataka Fikra zake zifanye kazi kwenye Kizazi Cha sasa, lazima itakula Kwao. Kuna Namna ya Kukifikia Kizazi Cha Sasa katika Kuihubiri Injili,Inawezekana kabisa Kizazi Kilichopita Kisielewe saaana Kile Kinachoendelea kwenye Kizazi cha Sasa lakini Usimuhukumu mtu kwa sababu ya Muonekano, Sababu ya Lugha, Sababu ya Mfumo wake Wa Maisha ila Muhukumu Sababu Ya Ile Kazi ya Msalaba Inayotenda Kazi ndani Yake". Haya ni baadhi ya Maneno aliyoyanena Mtumishi wa Mungu Bishop and Apostle Tumwidike jioni ya leo pale Mlimani City Hall.

Live Performance za Leo nadani kama kuna hakuna Majotro basi hii ndo ilikuwa hakuna Majotro ya Mwaka 2011. Mungu amezalisha Jambo kwenye Kizazi hiki, inawezekana kisieleweke kwa sasa lakini kama ambavyo hayakueleweka mengi hapo kabla lakini baadae yakaeleweka basi hili nalo ni mojawapo. Na kuweza kuendelea halihitaji sana mtazamo wa mtu mmoja mmoja analionaje kuhusu hilo jambo, Kama unalielewa Kanyaga twende kama Huelewi juu ya Hilo Nyamaza Ombea tuone tunakokwenda. Haya ni baadhi ya maneno Blog imewanasa wadau na kuongea nao siku ya leo.

Siku ya Kesho Jumapili hapo Mbezi Mambo yatakuwa si Mambo "Tshirt na Jeans" sijui itakuaje.
Hii Dancing Group Ilifunika Mbaya na kitu kama Ya "Street Dancing"

Full Kazi.


Blog ikampata kwa Karibu zaidi huyu Jamaa anacheza Mbayaaaaaaaa.

Kulia aliyenyanya Mikono ni Mama wa Isaac Malonga na Mwenye Suti ni Baba wa Isaac Malonga...Hawa ndo Wazazi wa Mbeba Maono.

Kichwa Kimojawapo Cha Watanzania Apostle Onesmo Ndegi "Spiritual Father" wa Isaac Malonga akiwa ndani ya Nyumba.

Tangu nimfahamu Isaac leo ndo Nimemuona amevaa Suti, Mbeba Maono Pastor Isaac Malonga akiteta Jambo ndani ya Ukumbi.



Picha Tatu za Juu zinaonesha Living Water Worship Team wakiwa Jukwaani, Hiki Kikosi Kimebadilika sana Uimbaji, Upigaji, Uchezaji na Mwendo umekuwa kutoka Utukufu hado Utukufu.

Bibi Harusi Mtarajiwa Nsia Mlula akiwa ndani ya Ukumbi, hii ni Asset Mojawapo ya Ukweee.
Wadau wa Blog...Happy Donarld akiwa nani ya Nyumba.

Living Water


Mmoja wa Wasanii Walioshiriki RIOT mwaka huyu. Jamaa alikata Mistari Ya Kutosha sana.

Huyu dada alinitumia Vocal Moja ya Hatari sana.

Wadau wa Blog, John Melele akiwa na Keziah kwa Nyuma anayeonekana.

Mdau Mkubwa wa Blog, Kichwa Cha Ukweli Samuel Ndandala, Mtoto wa Mtumishi ndani ukumbi.

John Lissu akiwa na Mkewe Wakicheza Ndani ya RIOT Event.

Wadau wa Blog Neema na Shosti wake wakiwa ndani ya RIOT.

Kama Haukuja Hupaswi kuambiwa Kila Kitu fanya Hima Uje kesho.

Si Kitoto Event Ya Jana Hawa Wadau wa Tehillah wakifanya Kweli leo Jioni.

Blog ikamnasa Upendo Kilahiro akiwa na Binti yake ndani ya Ukumbi.

Blog ikawanasa Flora Mbasha na Mumewe Emmanuel Mbasha.

David Robert akiwa na Mkewe.

The Saints wakiwa tayari kushambulia Jukwaa.

The Saints wakikamua Kisawa Sawa.

Wageni Waalikwa wakiwa hawaamini Makamuzi ya Gospel Music.Mwenye Suti Ya Blue amekunja nne ni yule Mkali wa Gospel Music wa South Africa aliyepata tuzo mwaka huu Benjamin Dube.leo Dube Makamuzi kwenda Mbele.

Huyu Jamaa ali-tabiri Mbaya hii Group inatoka Kenya.

Every Body Put Your Hands Up.

Kenyans Group akifanya Kweli.

Isaac akimtambulisha Apostle Onesmo Ndegi pamoja na Mke wa Apostle Ndegi Lilian kwa namna ambavyo wamekuwa ni zaidi ya Wazazi wake wa Kiroho kwenye maisha yake.

Isaac akiwatambulishwa Wazazi wake Mr and Mrs Malonga.

Hawa ni Watenda Kazi Pamoja na Isaac ambao wamemfikisha hapo kushoto ni Irene ambaye ni dada wa Isaac, anayefuata ni Apostle Msoka Mume wa Irene, Pastor Mathias pamoja na Mke wake Agness. Hawa watu ndo wamekuwa wakifanya huduma hii ya Tehillah hapa Tanzania. Apostle Msoka na Irene wako mkoani Mbeya.

Kuna Machine, Kuna Vifaru, Kuna Matinga Tinga, Kuna ma booldozer kwenye Utumishi wa Kristo basi hili linaweza kuwa "Tinga Tinga Anointing". Isaac akamtambulisha Bishop and Apostle Tumwidike. Niliwahi andika zamani kuhusu Apostle huyu. Mimi Binafsi Salute sana hapo kwa Apostle. Leo Jioni aliongea maneno mazito sana ili uweze kuyaelewa lazima uwe na mambo mawili, Moja lazima usiwe na Ukakasi wa udini ndani yako ili uweze kuoelewa kinachoendelea ndani yako, lakini Cha Pili lazima level yako ya Kiroho isiwe chekechea. Aliongea Concept ya Wokovu kwenye maisha ya Mtu na Mind Of Christ in a Believer.

Hawa Jamaa si tu kwamba wanapiga beat za South wanakotoka bali wana zi feel hizo Beat za South.

Mojawapo ya Group ikifanya kweli leo Jioni.

More Pictures will be sent Baada ya Tukio la Kesho Pale Mbezi, Kile alichofanya Benjamini Dube.

No comments:

Post a Comment