Friday, September 16, 2011

Hali ya Ajali Ilivyo huko Zanzibar

Meli ya Mv Spice ambayo ilipata ajali usiku wakuamkia Tare 10/9/2011 imetuachia majonzi mengi katika taifa letu la Tanzania.Ni watu wengi wamepoteza maisha pamoja na Nduguzao.Meli hiyo ilitengenezwa mwaka 1967 nchini Ugiriki.Ilipo kuja Zanzibar ilipewa majina mawili,Lakwanza Apostolos P,na baadae kuitwa Mv Spice Islander.
Hii ndo Meli Mv Spice islander.Picha hii ilipigwa Mwaka 2007 ikiwa Zanzibar.

Hali ya uwokoaji huko Nzanzibar imekuwa ikiendelea lakini kwamujibu wa Ripota wangu wa Blog hii Baraka Malya alioko eneo la tukio,anasema hali ningumu sana kwani sehemu iliopata ajali Mv Spice nisehemu yenye kina kirefu sana na Mvutano wa maji na Ang'aa,Ivyo kuwapatabu waokoaji waliotokea South Africar.
Waokoaji wa South Africar wakiwa wamemuokoa Mtoto.
Baadhi ya Watoto wadogo walio bebwa wakiwa wamesha poteza maisha.
Hivi unavyo viona kama vitu vimekusanyika nibaadhi ya watu wakisaidiwa kufika ng'ambo.
Hawa ni ndugu walio kalia Godolo.Godolo likiingia maji halizami bali linaelea.Nakuna walioshika Mifuniko iliyojaa vile viatu vya yeboyebo nawao kuelea kwenye maji,na wengine walitumia Milango ya Mbao n.k.Katika kujiokoa
Baadhi ya watu wakiangalia Picha zilizopingwa kwajili yakuwatambua ndugu zao.
Hivi ndivyo ilivyo pinduka Meli ya Mv Spice.
Wakazi wa Kisiwa cha Unguja wakishirikiana na wanajeshi katika zoezi la uokoaji wa watu walionusurika ajali na Maiti mbalimbali zilizo patikana.
Makaburi yaliochimbwa Zanzibar kwajili ya Maiti ya waliofariki katika ajali ya meli MV SPICE ISLANDER.

Picha hizi kwa hisani ya ripota wangu Baraka Malya alioko Zanzibar.

No comments:

Post a Comment