Saturday, October 15, 2011

MAPINDUZI YA SIFA NA KUABUDU YAFANYIKA JIJINI MWANZA

Ilikuwa ni Siku ya kupendaza sana ambayo wengi hawakutegemea kama ingekuwa hivyo na kwa wewe uliyekosa pole sana kwani umekosa kitu kikubwa sana kwenye maisha yako ya kiroho na kimwili.


Ni Mchanganyiko wa waimbaji wote wa Jiji la Mwanza wakiongozwa na New Life Band kutoka Arusha katika jukwaa moja kwa lengo moja tu la kusifu Kumwabudu Mungu.


Angalia mambo yalivyokuwa kuanzia wakati waufungaji wa vyombo siku moja kabla
Hapa ilikuwa wakati wa kuset vyombo
Mzee watumba Deo nae hakuwa nyuma kuhakikisha kila kitu kinakwenda poa
Jimmy Akijaribu Keybord kama iko poa siku moja kabla
Huu ulikuwa ni wakati wa majaribio watu waliserebuka ile mbaya

Kabla ya kupanda jukwaani ilikuwa ni nafasi ya kukutana kwa mara ya mwisho na kufanya maombi ya pamoja




Prince Adolph Nzwalla Mtangazaji wa HHC ALIVE FM 91.9 Ya Jijini Mwanza wakwanza kushoto akiwa na waimbaji wa New Life Band kabla ya kupanda Jukwaani.
Abedinego wa New Life Band Akitoa Maelekezo kwa Waimbaji Wa Mwanza Mass Choir

New Life Band Wakiingia Jukwaani wakiongozwa na Mkurugenzi Mabondo maarufu kwa jina la Ondo
New Life Band Wakiwa Jukwaani kuanzisha Mapinduzi ya Sifa Na kuabudu ndani ya viwanja vya furahisha Jijini Mwanza
Smith Swai (Mukubwa King Presenter) Mtangazaji wa Radio Ya Kikristo Jijini Mwanza ya HHC ALIVE FM 91.9 Watatu kutoka kushoto mwenye Suti nyeusi Dakika za mwisho kabla ya Kupanda Jukwaani
New Life Band Walianzisha Ibada kwa stail ya vocal kavu bila ala yoyote ya Muziki, kiukweli ilikuwa nzuri sana na ilipendeza kupita maelezo.
Baada ya New Life Band Kupanda Na kuanzisha Mwanza Mass Choir nao walipanda wakiongonzwa na Martha Turtis Mmoja wa waimbaji wanaokuja kwa kasi katika ulimwengu wa Gospel song


Eglah akikandamiza Drums Nyuma yake Mwanza Mass Choir wakiendelea Kukamua

Baraka wa Huima Band katika Drums

Japhet wa Uhima Band nae hakuwa nyuma katika kuhakikisha ibada inakuwa ya viwango vya ubora
Mungu aliwagusa watu kupitia sifa na kuabudu

Jukwaa lilikuwa Dogo Baada Mambo kunoga Ilibidi Mass Choir Washuke Chini Ili Jukwaa lisije likashuka maana moto uliwaka mpaka Wachungaji na Maaskofu waliokuwepo wakakosa la kusema.

Mwenyekiti wa Umoja wa makanisa Askofu Sekelwa Nae alikuwepo

Prince Adolph Nzwalla katikati nae hakuwa nyuma katika kulishambulia jukwaa

King Presenter Wa HHC ALIVE FM 91.9 nae hakuwa nyuma kumtukuza Mungu



Abednego wa kwanza Kushoto, King Presenter Smith Katikati na Prince Adolph wakiwa jukwaani wakimtukuza Jehova

G. Sengo Wa Clouds Fm Mwanza Nae hakuwa nyuma ktk kumsifu Mungu

Waimbaji wa Mwanza Mass Choir Kutoka Hosanna Praise Team Kilimahewa

Abedinego wa New Life Band Akiwa na mke wake wakishambulia Jukwaa.


Ebwanaa eeeeee watu walikuwa ni wengi ile mbaya.

New Life Band Hawakuwasahau wachungaji na Maaskofu waliokuwepo kutoka kushoto ni Bishop Isaya, Bishop Swai, Bishop Sekelwa na Bila kumsahau Bishop Batenzi.


Bishop Swai Akifunga Ibada hii y Sifa N a Kuabudu Kwa Maombi

No comments:

Post a Comment