Monday, October 3, 2011

Neno La Faraja

Yawezekana umepita katika hali ngumu ya maisha, kiasi kwamba umetamani usingekuwepo au upotee urudi mambo yakiwa safi, wakati mwingine umejuta na kusema laiti kama nisingezaliwa labda kwa vile huna wazazi au umeumizwa na mpendwa wako au umewapoteza watu uliokuwa ukiwategemea na mara zote unadhani hakuna anayekupenda wala kukujali. Utakapowaza haya hakika hutakuwa na furaha, na ndio maana unajribu kutafuta furaha sehemu nyingi lakini bado mawazo yanarudi palepale. Napenda kukuhakikishia mpendwa unayesoma hapa, yawezekana ukapata furaha na amani kwa maana hauko peke yako. Yesu anakupenda na anakuwazia mema kumbuka kumkaribisha moyoni mwako ili awe rafiki yako. Yeye ni rafiki wakweli wengine wanakucheka wanafurahi jinsi unavyoshindwa lakini Yesu atakupitisha katika majaribu yote kwa maana majaribu tunapitia ili tuweze kufika pale Mungu anapotaka majaribu ni mtaji au ni mtihani ili kushinda inabidi kupitia hayo. Mungu anakupenda anajua kila unachohitaji chukua hatua sasa jifunze kuomba mwenyewe, ukimwambia Mungu siri wa moyo wako hakika utaona faraja na utapata FURAHA ya kweli.

No comments:

Post a Comment