Monday, April 9, 2012

Kanumba Kuzikwa Dar Kesho


Taarifa iliyotolewa jana jioni na mmoja wa wana kamati ya mazishi, Hidi Mchome, ilisema kuwa Kanumba atazikwa kesho katika makaburi ya Kinondoni majira ya saa 10 alasiri. Uamuzi huo ni baada ya ndugu zake kuwasili akiwemo mama yake mzazi na kwamba salamu za mwisho za kuuaga mwili wa marehemu zitatolewa katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa nne asubuhi. Mama wa marehemu , Flora Mutegoa amekubali mwanae azikwe kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Mchoma alisema baada kuwasili kwa mama mzazi wa Kanumba amekubali shughuli za mazishi zote zifanyike hapa Dar es Salaam.Mama huyo aliwasili jana saa nane mchana akitokea Bukoba, baada ya mama huyo kuwasili aliibua vilio upya kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki, huku dada yake Kanumba Abela Kajumulo akizimia muda mfupi baada ya mama yake kuwasili nyumbani hapo. wakati anawasili Sinza, nyumbani ya marehemu Kanumba ilizungukwa na umati wa waombolezaji, waliokuwa ndani walitoka kumpokea na hata wale waliokuwa jirani na eneo hilo walisogea wakitaka kumuona. Kuwasili kwa mama huyo kuliongeza machungu kwa ndugu, jamaa, wasanii na mashabiki ya msanii huyo nguli kiasi cha baadhi yao kupoteza fahamu. Katika siku tatu za maombolezo , mamia ya watu wa kada mbalimbali wanafika nyumbani kwa marehemu kuwafariji ndugu na jamaa zake.Kutokana na eneo hilo kuwa na idadi kubwa ya watu,Waombolezaji kadhaa wamekuwa wakizimia, lakini watu wa huduma ya kwanza walifanya kazi kubwa kuwasaidia. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limeimarisha ulinzi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuifunga kwa muda barabara ya Sinza-Magomeni eneo la Vatican Rais Jakaya Kikwete jumapili aliongoza mamia ya waombolezaji katika msiba wa msanii huyo akisema alilazimika kusitisha safari yake ya nje ya nchi ili kuungana na wananchi wengine katika maombolezo hayo. Rais Kikwete aliwasili nyumbani kwa marehemu Kanumba majira ya saa 6.35 mchana na kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huo. “Nimeguswa na msiba huu, nilikuwa nisafiri lakini nimeamua kuja hapa kuwapa pole ndugu na wasanii wote,” alisema Rais. "Nilipata taarifa za msiba jana asubuhi, nimezipokea kwa mshtuko mkubwa taarifa hizi, naombeni muwape familia ushirikiano unaostahili msiwaburuze, waacheni waamue watakapompumzisha ndugu yetu, alisema Rais Kikwete. Nakumbuka mara ya mwisho nilionana naye Dodoma mwaka jana nilipokula chakula cha mchana na wasanii tulizungumza mengi, amefariki mapema mno, akiwa bado na umri mdogo, mwenendo wake ulikuwa mzuri tumepoteza mtu muhimu katika tasnia ya sanaa." Rais Kikwete alisema "Nilitaka kuongea na nyinyi, lakini nimekosa kipaza sauti, mambo niliyokwisha panga na wasanii yataendelea nayo, kikubwa ni kuona wasaniii wanafaidika na kazi zao, hamu yangu ni kuona wanafika viwango vya kimataifa. Kuna kazi niliwapa wasanii wafanye na waniletee ripoti kwa kweli kama serikali hatuna pingamizi kwa suala la vifaa na fedha nipo tayari kuzitoa kwa ajili ya kuinua wasanii, kwani wanafanya kazi kubwa, lakini wanapata kipato kidogo, kama serikali tutashugulikia suala hilo."alisema kuwa Kanumba alikuwa ni msanii anayependa maendeleo ya wengine ndiyo maana alijitolea kuwainua baadhi ya wasanii. Aliwataka wasanii wenzake kuuenzi utaratibu huo ili nao waje wakumbukwe pindi watakapoondoka katika uso wa dunia. Rais Kikwete aliwataka wafiwa wawe na subira huku wakiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu ya kukabiliana na hali ngumu waliyonayo ya kuomdokewa na kipenzi chao MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, imetoa rambirambi ya sh milioni 1 kwa familia ya aliyekuwa msanii huyo mahiri hapa nchini. Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine, alisema wameamua kutoa kiasi hicho kidogo, ili kiweze kusaidia katika mambo mbalimbali msibani hapo. Msafara wa Yanga msibani hapo mbali na Mwesigwa, wengine waliokuwepo ni Salum Rupia na Ally Mayai, ambao ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Ofisa Habari, Louis Sendeu, sambamba na nyota wa kimataifa wa klabu hiyo, Waghana Yaw Berko na Kenneth Asamoah.Kwa upande wake, Asamoah alisema aliposikia msiba wa msanii huyo hakuamini, kutokana na jinsi ambavyo alimuona siku ya sherehe za Kombe la Kagame zilizofanyika ukumbi wa Nyumbani Lounge, mara baada ya Yanga kuibuka mabingwa mwaka jana. “Mimi kifo cha Kanumba kiukwweli kinaniuma sana, maana nilikuwa nikimuona katika filamu mbalimbali, lakini nikaja kumuona siku ya sherehe za Kombe la Kagame, Mungu amlaze mahali pema peponi amen,” alisema Asamoah huku machozi yakimtoka Kanumba aliyefariki ghafla baada ya kudaiwa kuanguka akiwa ndani kwake na mpenzi wake, Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu (18), taarifa za kifo chake zimekuwa na mkanganyiko ambapo baadhi ya watu wanadai kuwa alinyweshwa sumu na wengine wakisema alipigwa na kitu chenye ncha kali kisogoni. Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, jana lilitoa taarifa ya uchunguzi wa awali likisema kuwa mbali na maelezo ya mdogo wa marehemu, Seth Bosco (24), pia panga, pombe aina ya ‘whisky’ ikiwa robo glasi na soda aina ya sprite vilionekana chumbani kwake.Akifafanua zaidi kuhusu chanzo cha kifo cha Kanumba, Kamanda Kenyela alisema kwa mujibu wa mdogo wake, Bosco, ambaye pia ni msanii wa kikundi cha The Great Filamu Production, siku ya tukio aliambiwa na kaka yake kuwa ajiandae ili amsindikize sehemu. Alisema kuwa baada ya kumweleza hivyo, Kanumba aliingia chumbani kwake kujiandaa na kwamba baada ya muda kidogo alimwita mdogo wake chumbani kuwa kuna mgeni, ndipo Bosco akamwambia akiwa tayari angemuona. Kamanda alisema kuwa muda mfupi baadaye Bosco anasema alisikia kelele ambapo kaka yake alikuwa akimtuhumu mpenzi wake Lulu. Kenyela alisema kuwa Bosco alieleza kwamba alisikia sauti ya Kanumba akimhoji Lulu: “Kwa nini unawapigia simu mabwana zako wengine?” Ghafla Bosco aliitwa na msichana huyo na kumuambia kuwa akamwangalie kaka yake amezidiwa. Bosco alieleza kuwa aliingia chumbani na kumkuta Kanumba amelala sakafuni huku akitokwa na povu mdomoni akiwa haongei. Alisema kuwa alitoka nje na kumwangalia Lulu, lakini hakumuona na hivyo kuamua kumpigia simu daktari wa Kanumba ambaye baada ya kufika aligundua kuwa amekwishafariki. Seth Bosco ambaye ana sura inayoshabihiana kwa karibu Kanumba alisema kauli ya mwisho kuisikia kutoka katika kinywa cha kaka yake huyo ilikuwa ni ‘nisubiri.’ Alisema jioni ya Aprili 6, mwaka huu, marehemu alimwambia angependa watoke kwenda matembezini pamoja. “Ilipofika sita za usiku, nilimwambia kuwa mimi nimekwishajiandaa, akasema ‘nisubiri’ na kisha akaingia chumbani mwake,” alisema Seth na kuongeza: “Kanumba akiwa chumbani kwake, aliingia binti mmoja, ambaye ninamfahamu kuwa ni mtu wake wa karibu. Kwa kuwa namfahamu, sikushangazwa na ujio wake, aliingia chumbani kwa Kanumba.” Seth alisema baada ya muda, alisikia sauti zilizoonyesha mgogoro wa aina fulani kutoka chumbani humo na alipotaka kuingia, mlango ulikuwa umefungwa kwa funguo. “Nilisikia Kanumba akimwambia Lulu; ‘Yaani unapigiwa simu na mwanamume wako mbele yangu?’ Baada ya dakika kadhaa za mzozo chumbani, Lulu alitoka akisema kuwa Kanumba ameanguka,” alisema Seth. Seth alisema ripoti ya awali ya daktari inaonyesha kuwa marehemu hana jeraha lolote katika mwili wake… “Kama alisukumwa ukutani, basi lazima jeraha lingeonekana katika ubongo, lakini ripoti inaonyesha hana jeraha na mimi nilimkuta marehemu akiwa anatokwa na povu mdomoni, macho yamemtoka, huku akikoroma, cha ajabu hakutokwa damu… bado tunasubiri uchunguzi zaidi wa polisi.” Akimzungumzia marehemu Kanumba, Blandina Chagula (Johari), alisema alikuwa zaidi ya rafiki kwake akisema hawakujuana katika maigizo tu, bali walicheza pamoja tangu utotoni. “Nimesoma na Kanumba Mwanza, Shule ya Msingi Bugoyi, lakini si hivyo tu, bali mama yake Kanumba na mama yangu ni marafiki wa karibu. Tulikutana tena hapa jijini, lakini yeye akisoma Shule ya Jitegemee mimi, shule nyingine, ndipo tulipojiunga katika maigizo katika Kikundi cha Kaole.” Johari alisema amepata pigo kwa kuondokewa na Kanumba kwani alikuwa ni zaidi ya kaka na zaidi ya rafiki akisema alikuwa mshauri na alimuonya pale alipokosea. Alitaja mambo matatu ambayo angependa wasanii wengine wamuige Kanumba. Aliyataja kuwa ni uchapakazi, kujihifadhi na ustaarabu…“Hana mfano wake, alikuwa ni mstaarabu, mwenye upendo na anayejiheshimu,” alisema Chagula. Ruth Suka (Mainda) ambaye aliwahi kufanya kazi na marehemu Kanumba pia alimwelezea kuwa alikuwa miongoni mwa watu wachapakazi na wanaojiheshimu. Alisema Kanumba alikuwa kijana mstaarabu na kabla hajawa maarufu, alikuwa akiogopa mno kuwa karibu na wanawake… “Ni mtu aliyejisitiri mno na mambo yake, lakini mazingira yake ya usanii yalimfanya aanze kuchangamka na kujichanganya na watu wa rika zote. Kwa kifupi ni mtu wa kanisa.” Msanii mwingine ambaye pia alisoma na marehemu Jitegemee, Emmanuel Myamba alisema alikuwa na uhusiano wa karibu na kwamba alifahamu mambo mengi na kujifunza mwengi kupitia kwa marehemu. Aprili, 6 mwaka huu Kanumba alitoa ujumbe ulioonekana kutabiri kifo chake, akiyanukuu maneno ya Mwanafalsafa, Albert Pine yaliyosema: “Tunachofanya kwa ajili yetu tunakufa nacho. Lakini tunachofanya kwa wengine na kwa ulimwengu, kinadumu na ni cha milele.” Mara ya mwisho Kanumba anaongea na mama yake mzazi ilikua alhamisi jioni na alikua anamsisitizia Mama awahi kwenda Dar es salaam kwa sababu anasafari ya kwenda Marekani Alhamisi ijayo ambapo mama yake alikua amekata ticket ya kwenda Dar es salaam baada ya pasaka mama mzazi wa STEVEN KANUMBA amekanusha taarifa zilizoenea kwa baadhi ya watu kwamba Kanumba hana ndugu. Amesema “ni waongo tu, mimi ndio mama yake mzazi kuna dada zake, kuna ndugu kama unavyowaona hapa na Dar es salaam wako wengi tu wamekusanyika, alieamua kutangaza katangaza kivyake tu”kauli hizo alizitoa kabla hajawasili Dar Es Salaam

No comments:

Post a Comment