Wednesday, April 25, 2012

Wednesday, April 25, 2012

Askofu Gwajima Ziarani Jijini London


Askofu Josephat Gwajima akihubiri jijini London Mwaka jana mwishoni
Mchungaji Josephat Gwajima  wa kanisa la Glory f Christ Tanzania anatarajia kuwepo jijini london kuanzia jumapili hii ya tarehe 29 hadi tarehe 6 ya mwezi wa tano.kwa yeyote ambaye angependa kukutana na mchungaji kwa ajili ya maombi na ushauri basi anatakiwa kupiga simu namba 
0742 7532044 au
07429667095
ili kupanga siku na muda ambao angekutana na mchungaji.
Pamoja na hayo mchungaji atakuwa kwenye tawi la kanisa lake jumapili zote mbili kwa yeyote ambaye angependa kufika afuate anuani hii
Glory of christ ministries international,
langham road,Tottenham,
London, N15 3RB.
Kwa Maelezo zaidi unaweza piga simu kwenye namba tajwa hapo juu.

Paty attah na Eucharia Anunobi Ma-staa wa Nigeria waliompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha Yao


Paty Attah
Paty attah ni raia wa Nigeria na mmoja kati ya wakongwe wa tasnia ya filamu nchini humo , kwa miaka ya hivi karibuni, Paty amempokea kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Baada ya kuokoka, amekuwa akijituma katika kuwarudisha watu wengi kwa kristo kupita njia mbalimbali pamoja na kushare maneno ya Mungu katka wall yake ya Facebook na Twitter
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Nigeria Paty kwa sasa anaishi jijini Humburg nchini Ujerumani na tofauti na utumishi, Paty ni muigizaji wa Filamu kazi ambayo anaiendeleza nchini humo .Pamoja na hayo pia ni mwanamitindo na Mwanamuziki. Paty mpaka sasa ameshacheza zaidi ya filamu arobani zikiwemo Secret Fantasy, Final Spirit of Love, Fools in Love, More than Gold, Only Love pamoja na  Songs of Sorrow.


Eucharia Anunobi
Kama kuna watu ambao waliwahi kuushangaza uma wa wanigeria kwa kauli zao kuwa wameamua kuokoka basi Eucharia Anunobi ni mmoja wao,Eucharia  maarufu kama UK, alikuwa ni mmoja wa ma-staa wa Nollywood waliojulikana sana hasa kwa mtindo wake wa kuvaa nguo huku sehemu kubwa ya kifua chake ikiwa wazi.
Kwa sasa UK ameokoka na amekuwa akihubiri na kumshuhudia Yesu pasipo kificho.Kuna habari za hivi karibuni zinasema ameamua kuwa mchungaji na amesimikwa rasmi kwa kazi hiyo hivyo kwa sasa anachunga kanisa lake.Eucharia alipata nafasi ya kuhubiri wakati wa kusimikwa u-shemasi mbunifu wa mitindo na muigizaji nguli nchini humo Clarion Chukwura’s

Tuesday, April 24, 2012

ZIARA YA UPENDO KILAHIRO NCHINI CANADA YAANZA KWA MAFANIKIO WATU WATATU WAMPOKEA YESU

Upendo Kilahiro akimsifu Mungu.
Mwimbaji nyota wa gospel nchini Tanzania Upendo Kilahiro ameweza kupokelewa vyema nchini Canada huku tamasha lake la kwanza kufanyika jijini Ottawa ndani ya kanisa la Christ Chapel Bible kufanyika kwa mafanikio ikiwa ni pamoja na watu watatu kukabidhi maisha yao kwa Yesu na mwengine akipokea uponyaji.

Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kwa ajili ya kukusanya fedha za umaliziaji wa shule ya watoto yatima ya mkoani Morogoro nchini Tanzania iitwayo Dayspring Orphanage boarding school ambayo inafadhiliwa na kanisa hilo,ambapo watu wengi walihudhuria wakiwemo kutoka makanisa ya jirani kama River Jordan Community kwakuwa ni kawaida makanisa jirani kusaidiana na kuwa pamoja kwenye matukio kama hilo,tamasha hilo liliongozwa na viongozi wa kanisa hilo akiwemo Bishop Afolabi,Peter Mwaiteleke huku wageni rasmi walikuwa maafisa ubalozi wa Tanzania nchini humo pamoja na Dada Niku Kyungu Mordi na mumewe ambao hufanya huduma ya kuhubiri huko Maryland Marekani. 

Upendo aliimba nyimbo mbalimbali na kuwabariki watu waliofika katika tamasha hilo,mwimbaji huyo ambaye si mara yake ya kwanza kuwa nchini Canada,pia mwishoni mwa mwaka jana yeye pamoja na waimbaji wenzake Christina Shusho na Upendo Nkone walikuwa nchini Marekani kwa ziara ya kumsifu Mungu. atakuwa nchini humo kwa ziara ya mwezi mmoja,huku mwimbaji mwingine Flora Mbasha na mumewe wakiwa nchini Marekani kwa ziara ya kumsifu Mungu.

Bishop Afolabi akimkaribisha Upendo Kilahiro kwa ajili ya kumsifu Mungu.

Hakika ngome zilianguka.

Mchungaji Peter Mwaitekele akipozi na Upendo kwa ajili ya picha.

Dada Edith Mwita mdau mkubwa wa gospel VIPAJI HALISI Canada ambaye ndiye aliyefanikisha habari hii akiwa kwenye picha ya pamoja na Upendo Kilahiro.

Zainabu mwanadada aliyekata shauri na kumpokea Kristo mwaka uliopita akipozi na Upendo.

Watoto waliguswa na uimbaji wa Upendo wakaomba sign yake.

Dada Edith Mwita,Zainabu pamoja na wanaigeria wakipozi kwa ajili ya kupata picha.

Hakika ilikuwa siku ya furaha .

Friday, April 20, 2012

''AHADI ZAKE'' WA MARION SHAKO WIMBO ULIOTOLEWA NENO LA KINABII KABLA HATA HAUJATUNGWA''

Marion Wyali Shako.
               

  ''Nafsi yangu usichoke roho yangu msifu Bwana aliahidi atatenda,mtumainie Bwana,ahadi zake     ni za milele akiahidi atatenda,roho yangu nafsi yangu mtumaini Bwana.

         Kama mvua ishukavyo toka mbinguni kwenye ardhi na neno lake kwa kinywa chake halitarudi bure,litatimiza ahadi zake litatenda alivyosema aliahidi atatenda mtumainie BWANA''


Hayo ni maneno katika beti la kwanza na kiitikio cha wimbo ''AHADI ZAKE'' wimbo ambao umetoka takribani miaka minne iliyopita lakini ukiendelea kubariki na kugusa watu wengi mpaka leo kupitia mwimbaji wake na mtunzi wa wimbo huo mwanadada Marion Wyali Shako,ambaye kitaaluma kasomea mambo ya utawala(Administrative Assistant)akiwa mwajiriwa katika moja ya ofisi huko Mombasa nchini Kenya.


Katika taarifa yake ambayo aliwahi kuitoa kupitia Wapo Radio Fm akihojiwa katika kipindi cha ''Safari ya jioni'' alisema wimbo wa AHADI ZAKE ambao upo ndani ya album yake ya ''MSAADA WANGU'' alipewa neno la kinabii na nabii Teresia Wairimu kwamba Mungu atampa wimbo utakaobadilisha maisha yake na watu wengine,wakati anapewa unabii huo alikuwa katika hali ya uhitaji sana na album yake hiyo mpaka anaifanikisha kuirekodi ni Mungu mwenyewe alimsimamia kwani alimaliza salio lake lote alilokuwa nalo na pia alipitia mapito magumu sana.


Lakini kama mtumishi wa Mungu alivyompa unabii ni kweli ikatimia wimbo wa ''AHADI ZAKE'' umebadilisha maisha yake na watu wengi sio Kenya tu bali sehemu mbalimbali duniani
Marion alipotembelea nchini Uingereza mwaka 2009,akiwa katika pozi na masanamu ya familia ya Prince Charles,mkewe Camilla pamoja na watoto wake Prince William pamoja na prince Harry.
Pia amepata mafanikio mbalimbali zikiwemo tuzo huku album zake zilizofutia nazo zimeendelea kubariki wengi.huo ndio wimbo wa ''AHADI ZAKE''kutoka kwa mwanadada Marion Wyali Shako ambaye licha ya kuwa ni mwajiriwa pia anajihusisha na biashara huko kwao Mombasa Kenya akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano wa mzee Aggrey na marehemu Sylivia Shako wakazi wa Mombasa nchini Kenya na ni muumini wa kanisa la Jesus Celebration Centre kwa askofu Wilfred Lai.





No comments:

Post a Comment