Wednesday, November 23, 2011

MKUTANO WA KUJIKOMBOA NA KUONDOA UMASKINI KUPITIA BIASHARA NA UJASILIAMALI NDANI YA ARUSHA


Band inayopiga muziki wa injili LIVE nchini Tanzania, Glorious Celebration ikiwa sambamba na Erick Shigongo katika mkutano utakaofanyika Arusha tarehe 27 Nov.2011 imejiandali kikamilifu kuwasha moto wenye kuchoma mapepo na kufungua akili za watakaohudhuria mkutano huo ili kuweza kupokea masomo yatakayofundishwa na mjasiliamali huyo.

MWISHO
--------------------------------------------------------------------
SOMO LA UJASILIAMALI KUTOKA KWA MJASILIAMALI MWENYE ELIMU YA MTAANI, ERICK SHIGONGO WA GLOBAL PUBLISHER AKISINDIKIZWA NA BAND INAYOPIGA LIVE MUSIKI WA INJILI, GLORIOUS CELEBRATION YA JIJINI DAR ES SALAAM

MAADA

JINSI GANI YA KUANZA BILA KITU NA KUMALIZA UKIWA NA KILA KITU

Kuna mambo mengi Erick Ssigongo alifundisha katika hoteli yake ya The Atriums iliyoko Sinza Afrikasana ambapo Glorious Celebration Gospel LiVE Band walimuunga mkono kwa kuimba nyimbo za injili za enzi hizo.

Kabla ya kuanza somo lake Erick Shigongo aliwaomba watu wa Mungu kusimama na kufungua kwa maombi.

Pia alielezea historia yake kidogo, kuwa alitokea Mwanza akiwa ana Tshs.200,000/- akielekea Dar es Salaam akiwa hajui atafikia wapin na kwa nani. Alipofika Dar es Salaam alianza kujibiidisha katika kazi na lkumuomba Mungu sana.

Erick Shigongo alionekana mwenye uchungu hasa pale alipojieleza kwamba yeye hakubahatika kusoma sana kama watu wengine walivyobahatika kufika vyuoni na sekondari. Ila anamshukuru Mungu sana kw kuunganishwa na mzungu ambaye alikuwa msaada mkubwa sana katika kujua kuzungumza kiingereza na alipenda sana kusoma magezeti ya kiingereza kama The Guardian, Observer ili kujenga kiingereza chake.

Mbali na hapo, alielezea maisha yake akiwa akiwa mwanafunzi, alisema alidharaulika sana kwani alikuwa hana akili akiwa darasani na kila akitaka kunyoosha mkono wake ili ajibu swali alibaguliwa. Shigongo alimshukuru Mungu kwa kumfikisha hapa ambapo leo hii watu wanamsikiliza mtu aliyebaguliwa na kudharauliwa na kuonekana mtoto wa mtaani na asiye na akili....

Erick Shigongo kwa sasa anamiliki kampuni ya uchapishaji magazeti na vitabu ya Global Publisher, anamiliki hoteli kubwa Dar es Salaam za The Atriums na kampuni nyingine nje ya nchi ya Tanzania.

Na sasa ngoja tuonna tujifunze kile alichadhamiria kukifundisha kwa Watanzania kama kijana wa mtaani asieenda shule:-


Shigongo alifundisha ni jinsi gani ya kuanza bila kitu na kumaliza ukiwa na kila kitu. Alisema inawezekana kwa kila mtu kuanza bila ya kuwa na fedha na baadaye akiwa kuwa na fedha tena nyingi tu.

Kuna mambo matatu ya muhimu katiika kufanikiwa
1.Wazo
2.Fedha
3.Watu

Mtu unaweza kuwa na wazo lakini ukakosa fedha, inawezekana ukawa na fedha nyingi lakini ukawa huna wazo kuhusiana na hizo fedha zako na pia ukawa na watu wakukusaidia au marafiki lakini wakashindwa kukusaidia kwasababu huna wazo au fedha. Kwahiyo hivi vitu vitatu viantegemeana.

Kwahiyo kinachotakiwa ni kuwa na kimojawapo na kukifanyia kazi ipasavyo ili mwisho wa siku uwenavyo vyote.

Ukiwa na wazo jaribu kulifanyia kazi na kushirikisha vizuuri na yule uyemjua atakusaidia hasa mwenye fedha au shirikisha watu wengine. Na kama una fedha lakini hujui utafanyia nini jaribu kutafuta watu wenye wazo nao watakusaidia.

Erick Shigongo, mbali na kufundisha njia za mafanikio, pia alifundisha baadhi ya vitu vya muhimu kuvifuata ili kuondokana hali ya kutokuwa na kitu (umasikini) na kwenda katika hali ya kuwa na kila kitu (Utajiri),

1.Kuweka ukweli katika akili yako (thruth)
2. Kujiamini (Confidence)
3.Weka malengo (Goals)

Kuweka ukweli katika akili yako
-Uondoe fikra mbaya zilizowekwa na watu ya kuwa jambo fulani haliwezekani na badala yake weka ukweli kuwa jambo hili linawezekana na anza kufanyia kazi
-Ondoa vitu vinavyokusababishia kufikiria mambo akili yako hayawezekani na yapo kwaajili ya watu fulani.
-Muda wote fikiria kufanikiwa na iamini kazi yako kuwa ni bora kuliko ya mwingine.
-Tafuta marafiki watakao kusaidia katika mipango yako na sio watakao kujazia uongo katika akili yako

Kujiamini
-Jiamini kwa kila jambo unalifanya au kulifikiria.
-Usikatishwe tamaa na watu, dunia hii imejawa na wakatisha tamaa kuliko wale wa kukutia moyo.
-Jitahidi kuwa imara na bila kutikiswa na yeyote yule.
-Kila kitu unafanya amini kuwa kitaleta mafanikio hata kama unaona haiwezekani.
-Acha woga unapochangia maada fulani iwe kwa mkubwa wako wa kazi au mdogo wako wa kazi.
-Usikatishwe tamaa na kumbuka vikwazo katika kazi yako vinakusaidia kupanua akili yako ya kufikiri. Matatizo ni changamoto ya maisha.

Weka Malengo
-Weka malengo ya siku, wiki, mwezi, mwana na miaka.
-Fuatilia malengo yako uliyoyaandika kwa kuyawekea alama ya vema (tick) kwa yale uliyofanikiwa.
-Hakikisha asilimia kubwa ya malemngo yako yamefanikiwa na yale ambayo hukuweza kufanikiwa kwa wakati unaotakiwa yatafutia suluhisho

Bwana Erick Shigono alimaliza kwa kuwashukuru wote waliofika na kuwaomba wajaribu kufika kila Ijumaa kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku katika hotel ya The Atriums ambapo atamalizia somo lake hili na na pia kuwashauri watu wapende sana Elimu kwa Ufunguo wa maisha na kumpenda sana Mungu na Mungu akubariki!!!
Baada ya somo kuisha Erick Shigongo aliungana na marafiki zake na kuendelea kuburudika na nyimbo za kizamani za injili zilizoimbwa na waimbaji kutoka band ya Glorious Celebration ya jijini Dar es Salaaam.

No comments:

Post a Comment