Friday, November 25, 2011

Swahiba Prosper Mwakitalima Apata Ajali, Azungumzia Ajali ilivyotokea.


Sina maneno ya kutosha kukueleza Mungu amemponyaje mdogo wangu, Swahiba Prosper Mwakitalima katika ajali mbaya iliyotokea siku ya jana maeneo ya Ubungo.

Ilikuwa ni saa 8 na dakika 2 nilipopokea simu ya mtu mmoja akiniuliza "wewe ni Papaa?, ndugu wa Prosper?" nikajibu "ndio" akaniambia kuwa "Prosper amepata ajali ya gari, na tunampeleka Amana Hospital". Niliishiwa Nguvu lakini nikajikaza kiume.

Baada ya nusu saa nilifika Amana Hospital nikiwa mtu wa kwanza ndugu wa Prosper kufika baada ya kupata ajali.

Niliingia ndani Prosper akiwa amelala amefumba macho nilipomuona moyo wangu ukainama sana, muhudumu akamwambia Prosper kuna ndugu yako amekuja. Neno la kwanza kutamka Prosper akasema "Nani amekuja? nikamjibu "Papaa", Akaniambia "Umekuja na Nani" nikamwambia nimekuja na dogo Joel, akasema "Dont Worry am Ok, Nimepona na Nitaendelea kuwa mzima" Nilistuka sana, tukiwa chumba Na. 12 Amana Hospital Mimi, Joel na Prosper "Tukaliitia Jina la Bwana", Prosper akasema "Papaa thank you for Coming My brother, niko pouwa and I have peace".

Tukatoka Amana Hospital kwa Msaada Mkubwa wa Dr. Kilemile na Pastor Joyce Nkone na wengine kwenda Muhimbili, tulipofika Hospital ya Rufaa Muhimbili tukaambiwa T-Scanning machine ni mbovu haifanyi kazi, Ok hospital ta Rufaa T-scanning ni mbovu??wakatushauri twende Regency Hospital tukaenda huko ili kunusuru Maisha ya Ndugu yetu.....Majibu yakaonesha hakuna Mfupa wa Damu iliyoganda ndani, ina maana amepata majeraha ya nje tu.

Tukarudi Muhimbili huku marafiki wa Prosper wakiwa kama 50 waliokusanyika kuhakikisha hakuna jambo linakwama huku wengine wakiwa kwenye maombi hapo hapo Hospital. Saa 3 usiku tukafanikiwa kupata kitanda Kibasila namba 16 Chumba namba 113. Prosper akatamani kupata Chakula kwa kuwa hakuwa amekula siku nzima.

Wakati anakula Chakula akaaanza kutueleza siku ya Jana ilikuaje na siku chache kabla ya Ajali ilikuaje.

"Siku chache zilizopita niliota ndoto tukiwa wengi tunaenda mahali, wakati tunakwenda akatokea nyoka kama chatu, nyoka mkubwa akaanza kutukimbiza, ajabu yule nyoka akawaacha wote akaanza kunikmbiza mimi, nikastuka kwenye ndoto. baada ya siku kama mbili nikaota tena, tuko mahali lile joka likatokea linanikimbiza safari hii sikukimbia sana nikasimama, nikaanza kushindana nalo, nikatumia Jina la Yesu, lile joka halikunidhuru sana sikufa ila kwa sababu ya kushindana likanisababishia maumivu. Niliamka nikaanza Kukemea hiyo roho. Siku Ya Jana niliamka nikiwa sina mpango wa kutoka nyumbani, nia yangu iikuwa ni kupumzika na kupanga baadhi ya issue zangu za Ujasiriamali, nilipotoka nje pale nyumbani kuna kama pori, ile picha ya Joka ikanijia nikajisemea kuwa Lile Joka litatokea njia hii, nikajichekea kisha nikaingia ndani, ghafla nikapokea simu ya kunitaka kwenda Airport kuna kazi, kwa sababu za kibiashara nikafunga safari na gari yangu. Wakati narudi kutoka Airport nikiwa kwenye foleni pale maeneo ya River Side nikawa naongea na Machinga ili kununua Charger ya Simu, wakati tunaongea ghafla nikaona ligari likubwa la mafuta limeacha njia linakuja tulipo, ile picha ya Lijoka ikanijia mara moja kwenye ubongo wangu Nikaliitia Jina la Bwana, nikitendo kisichozidi dakika 1, tangu kuliona gari na mimi kupata ajali, ingawa nilipata ajali yule machinga alifariki hapo hapo nilikuwa na Amani sana sana, nakumbuka tu tangu kupata ajali na mimi kuja kutolewa kwenye gari ilichukua kama nusu saa lakini nilikuwa na Amani Sana, nilipoulizwa una ndugu wa kumtaarifu nikawaambia tafuta namba ya Papaa, thats all".

Baadae Prosper akaniuliza "Mwana gari yangu ikoje kwa sasa" nikawambia "Kaka gari ni chuma Chakavu" akasema anatamani kuona picha ya gari, tulipomuonesha akafumba macho akamshukuru Mungu On the Spot, Real It was a Miracle.

Asubuhi ya Leo tumeonana na Prosper anaendelea vema sana sana.

Swahiba Prosper Mwakitalima akila Chakula usiku wa Jana.

Picha Zifuatazo Zinaonesha Prosper akieleza Mungu alivyomuonesha ajali na pia na Pia ajali ilivyotokea na kuiona





Hii ni Gari inavyoonekana kwa Sasa baada ya Ajali ambapo Mungu amemtoa Prosper.

Hapa Gari likiwa Zimaaaaaaaa enzi za Focus.

No comments:

Post a Comment